Biashara yako kiganjani, hata bila mtandao.

Kwa maduka na famasi Tanzania. Uza, fuatilia stoo na ona kila tawi kwenye simu moja. Kwa Kiswahili au Kiingereza.

Hivi karibuniApp StoreGoogle Play

12:30
NeatFlowBIASHARA

Uza. Ona. Kua.

Toleo 1.0.0

Imetengenezwa kwa
Maduka ya rejarejaMaduka ya uremboVipodoziFamasiMini maketiMaduka ya rejarejaMaduka ya uremboVipodoziFamasiMini maketiMaduka ya rejarejaMaduka ya uremboVipodoziFamasiMini maketiMaduka ya rejarejaMaduka ya uremboVipodoziFamasiMini maketi

Hata mtandao ukikata, biashara inaendelea.

Hakuna mtandao? Endelea tu. Kila mauzo yanahifadhiwa kwenye simu na stoo bado inapungua. Mtandao ukirudi, NeatFlow inatuma yote yenyewe.

12:30
Aah! Mtandao umekatika…
12:30

Kila kitu duka linahitaji, kwenye programu moja.

Shuka chini na uangalie simu. Kila sehemu ni skrini halisi ya programu.

12:30

Stoo na Bidhaa

Pata tahadhari kabla bidhaa yoyote haijaisha.

  • Tahadhari za bidhaa kupungua kila tawi
  • Tarehe za kuisha, za zamani zinauzwa kwanza
  • Hamisha bidhaa kati ya matawi kwa haraka
  • Mizigo inaongeza stoo tawi sahihi
  • Kuhesabu stoo kwa idhini
  • Matawi yote sehemu moja, au yalinganishe

Na mengine mengi.

Telezesha simu au gusa mada

Mambo madogo, tofauti kubwa.

  • 08:02Amefungua Kariakoo
  • 10:41Mauzo · Taslimu35,000
  • 13:15Amefuta mauzo18,000
  • 13:16Amefuta mauzo18,000
  • 20:05Amefunga siku

Jua nani amefanya nini

Ona siku ya kila mtu: mauzo, yaliyofutwa, marejesho, matumizi na saa aliyofunga. Kitu kisicho cha kawaida kinaonekana haraka.

Haziuzwi · siku 30 zilizopita

  • Manukato 100ml3 zimeuzwa
  • Mafuta ya nywele2 zimeuzwa
  • Siagi ya shea4 zimeuzwa
Kwenye rafuTSh 628,000

Ona bidhaa zisizouzika

Ona bidhaa zinazouzwa kidogo na pesa kiasi gani imekaa kwenye rafu, kisha ziwekee ofa.

Faida wiki hii

TSh 0

JttJnnJtnAlhIjuJmoJpi
PDFExcel

Ripoti

Faida na hasara, bidhaa zinazouzwa zaidi, wafanyakazi na matawi. Pakua PDF au Excel.

Malengo ya mwezi

Weka lengo la mauzo la mwezi na uone unahitaji kiasi gani kila siku kulifikia.

Lipia unachotumia tu.

Chagua mpango, au jitengenezee wako kwa huduma unazohitaji. Kila bei inahesabiwa kwenye seva yetu, kwa hivyo jumla unayoiona ndiyo unayolipa.

Tunapakia bei…

Mambo watu hutuuliza.

  • Ndiyo. Endelea kuuza kama kawaida: mauzo yanahifadhiwa kwenye simu na yanajituma yenyewe mtandao ukirudi. Vitu vinavyohitaji mtandao tu, kama risiti za WhatsApp na ripoti mpya, vinasubiri hadi urudi mtandaoni.

  • Hapana. Kila mauzo, ufutaji na urejeshaji yanahifadhiwa na jina la aliyefanya, na hakuna kinachofutwa kabisa. Marekebisho ya stoo yanahitaji idhini ya mtu mwenye ruhusa kamili.

  • Ndiyo. Kila tawi lina stoo na mauzo yake, unaweza kuhamisha mzigo kati yao, na unaona matawi yote kwa pamoja au moja moja.

  • Ndiyo. Kila mtu anaingia kwa PIN yake na anaona tu ulichoruhusu, kwa mfano kuuza lakini si ripoti.

  • Duka lako haliko kwenye simu, liko kwenye akaunti yako. Ingia kwenye simu mpya na utakuta stoo, mauzo na wafanyakazi wako wote. Unaweza pia kuitoa simu iliyopotea kwenye akaunti.

  • Ndiyo. Kila kitendo kinafungamana na akaunti ya mfanyakazi, ruhusa zinawekwa kwa cheo ili mhudumu asione unachokiona wewe, na kumbukumbu zako zinabaki zako.

Bado una swali? Ongea nasi.

Jumatatu–Jumamosi, saa 2 asubuhi – saa 2 usikuDar es Salaam, Tanzania

Kuwa wa kwanza kwenye NeatFlow.

Acha namba yako. Tutakupigia au kukutumia WhatsApp nafasi yako ikifunguka. Hatutakusumbua.